KUFUATIA varangati lililotokea Tabora katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014, baada mpenzi wa mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kukataliwa na mashabiki, Shilole ameamua kufunguka kuwa Nuh atabaki kuwa mpenzi wake katika hali yoyote.
Mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akizungumza na paparazi wetu, Shilole alisema lengo lake lilikuwa ni kumtambulisha mpenzi wake kwa mashabiki wake japo walimkataa kuwa shemeji yao.
‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake ‘Nuh Mziwanda’.“Wakati namtambulisha Nuh kwa wakazi wa Tabora kuwa shemeji yao kiukweli nilishindwa kuelewa kwa nini nilizomewa ila ninachoweza kusema tena wakubali, wakatae Nuh atabaki kuwa shemeji yao tu,” alisema Shilole.
ConversionConversion EmoticonEmoticon