Taarifa kuhusiana na mastaa mbali mbali
ikiwemo wa muziki, filamu, na michezo kuingia katika headline
zinazowazungumzia kujihusisha na siasa sio taarifa ngeni kuzisikia,
ambapo kwa sasa mastaa wa movie wanaingia kwenye headline nyingine ya
wao kwa wao kugombea nafasi ya ubunge kwenye jimbo moja kupitia vyama
tofauti.
Mastaa wa filamu kutoka Nigeria Bob
Manuel Udokwu na Tony One Week Muonago wanaendelea kuzungumziwa sio kwa
sababu wamejiingiza kwenye siasa, bali kinachozungumziwa ni kitendo cha
wao kugombea nafasi hiyo katika jimbo moja kitu ambacho kimeanza
kuvutia hisia za watu wengi.
Bob Manuel Udokwu anagombea kupitia
chama cha APGA na Tony One Week Muonagor anagombea kwa tiketi ya ACN
katika jimbo moja la Anambra, Nigeria ambapo uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
unatarajiwa kufanyika katikati ya mwaka 2015, ambapo staa mwingine wa
Nollywood ambaye alitangaza kujiingiza kugombea ubunge ni Desmond
Elliot.
ConversionConversion EmoticonEmoticon