NI SHEEDAH 'WEMA, AUNTY.....................................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Ni sheedah! Pamoja na kukanusha kwa kutumia nguvu kubwa, nyuma ya ushosti wa mastaa grade one wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Aunty Ezekiel kuna siri nzito ikidaiwa kwamba wawili hao husagana.Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Aunty Ezekiel wakidendeka hadhalani.
TUKIO BICHI
Madai hayo ya muda mrefu huku wenyewe wakisisitiza si ya kweli, yameibuka upya juzikati baada ya warembo hao kuonesha mahaba niue au nikongorowe kisha ‘kudendeka’ hadharani na kusababisha mwandani wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kukasirika na kuondoka eneo la tukio akiambatana na timu yake ya Wasafi Classic Baby (WCB).
ILIKUWAJE? Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri usiku wa kuamkia Oktoba 28, mwaka huu ndani ya Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar ambapo Aunty alikuwa akisherehekea siku ya yake ya kuzaliwa ‘bethidei’.
WEMA ATOKEA DUBAI
Shughuli hiyo ilitawaliwa na matukio baada ya Wema kuwasili ukumbini hapo akitokea nchini China kupitia Dubai alikokwenda hivi karibuni kwa biashara binafsi ikidaiwa kwamba amerejea na mkwanja wa kutosha.
Wema alitinga ukumbini hapo saa 7:15 usiku na kuwakuta wadau wakiendelea na sherehe hiyo ambapo mara tu baada ya kufika alikumbatiana kimahaba na  Aunty zoezi lililochukua dakika kadhaa wakiwa wamenasiana huku wakifunika nyuso zao kwa zile nywele nyingi za Wema hivyo kilichoendelea humo ndani hakikujulikana. Walipojifunua kwenye nywele ndipo ikabaini kwamba kumbe walikuwa ‘wakidendeka’ bila kujali wingi wa kamera.
WASHUTUMIWA
“Mungu wangu, leo mambo hadharani. Mbona ni sheedah? Yaani wanadendeka hadharani! Kwa vyovyote vile Wema na Aunty husagana,” alisikika mmoja wa waalikwa.
Mmoja wa waigizaji chipukizi alidakia: “Yaani utadhani wapenzi kabisa maana kila mmoja anaonesha hisia za kumisiana. Hawaogopi kuambiwa wanasagana? Haya bwana, yetu macho maana leo tutaona mengi. Vitendo kama hivi ni vya kulaaniwa vikali na kuwakumbusha kwamba wao ni kioo cha jamii.”
DIAMOND AKASIRIKA, AONDOKA
Kufuatia  hali hiyo, Diamond alionekana kukasirika na kushindwa kuvumilia hivyo aliamua kuwaacha wajinafasi kwa kuondoka ukumbini akiwa ameambatana na timu yake. Waalikwa waliokuwa ndani ya ukumbi huo waliendelea kupigwa butwaa na kitendo hicho hasa Diamond alipoamua kusepa huku nyuma Wema na Aunty wakibaki huru na kuendelea kufanyiana mambo ya kimahaba mara nyingine wakati wakilishana keki kwa staili ya njiwa.
AMANI LAMVAA AUNTY
Baada ya kuona hali hiyo, paparazi wa Amani aliyekuwa ukumbini hapo alimvaa Aunty na kumuuliza kwa nini ameamua kuonesha hali hiyo mbele ya kadamnasi ambapo alijibu hakuna mambo ya usagaji. Alisema hali hiyo ilitokea tu maana yeye na Wema ni marafiki ambao wameshapitiliza hivyo wamejikuta wakiwa kwenye hali hiyo bila wao kuona kama ni tatizo. “Kwani nani asiyejua kama mimi na Wema ni marafiki, suala la kukisiana ni jambo la kawaida kwetu.
MAMA LA MAMA  
Kwa upande wake mama la mama Wema aliishia kusema kuwa alimmisi sana shoga’ke na hakuna jambo la ajabu ambalo amelifanya juu yake maana wao ni marafiki kama marafiki wengine.
TUJIKUMBUSHE
Kwa muda mrefu Wema na Aunty wamekuwa marafiki ambapo kila mmoja hulala kwa mwenzake tena kitanda kimoja tangu Wema alipotofautiana na Kajala Masanja ambaye naye aliwahi kuhusishwa na masula ya usagaji na staa huyo mkubwa asiyechuja.
Previous
Next Post »