JACK CHUZ: ETI MUME ANIZUIE KUIGIZA, ANAANZAJE!

STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ amefunguka kuwa madai yaliyozagaa kuwa mumewe, Gadna Dibibi amemzuia kuigiza hayana ukweli kwani naye anapenda kumuona runingani.Jack alifunguka hayo alipokuwa akijibu swali la paparazi wetu lililodai kuwa mume wake amempiga mkwara asiigize kutokana na wivu.
“Wee, eti anizuie kuigiza anaanzaje kwanza? Mume wangu alinikuta niko katika kazi hiyo, anapenda kuona naigiza, ananisapoti sana na hivi karibuni naachia kazi yangu mpya,” alisema Jack.
Previous
Next Post »