LUCY KOMBA: NIMEISHI NA MR. WIKI MBILI TU!

MSANII mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Lucy Komba amefunguka kwamba baada ya kufunga ndoa  hivi karibuni ameishi na mumewe Janus kwa wiki mbili tu.
Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Lucy Komba akiwa na mume wake mumewe Janus.
Akizungumza na paparazi wetu, Lucy alisema kwa sasa amebaki Bongo peke yake ikiwa ni baada ya mumewe kwenda kwao Denmark ambapo alitakiwa kurudi kazini lakini bado anafanya maandalizi ili amfuate.
“Mume wangu alikaa kwa wiki mbili tu baada ya kufunga ndoa nikamwambia aniache ili nimalizie kufanya maandalizi ya kumfuata huko kwao Denmark ambapo mpaka sasa sijajua nitaenda lini maana bado sijamaliza mambo yangu ila tunaaminiana na tumeshazoea kwani tangu wakati wa uchumba tulikuwa tuko mbalimbali lakini nitaenda.
Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Lucy Komba akipozi.
“Nikienda huko nitakaa kwa miezi mitatu nitarudi hapa Bongo kusalimia na kukaa kama wiki kadhaa, nampenda sana mume wangu na ninammis kwa kweli,” alisema Lucy Komba.
Previous
Next Post »