KADINDA AMUANIKA MPENZI

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda ameamua kumuweka wazi mpenzi wake ambaye siku za nyuma alikuwa na mpango wa kufunga naye ndoa mapema mwaka huu lakini kukatokea tofauti kidogo wakahairisha zoezi hilo.
Mwanamitindi maarufu Bongo, Martin Kadinda akiwa na mpenzi wake.
Akizunguza na  mwandishi wa habari hivi karibuni, Kadinda  aliweka wazi kuwa huyo ndio mke wake mtarajiwa na Mungu akipenda watafunga naye ndoa mwakani.  “ Ni kweli ni mpenzi wangu nampenda sana na Mungu akipenda ndiye mke wangu ambaye nitafunga naye ndoa mapema tu mwakani na Mungu atusimamie katika hilo,” alisema Kadinda.
Previous
Next Post »