Mtu mmoja amekatika miguu na wengine
kujeruhiwa vibaya baada ya lori moja kugongana uso kwa uso na gari la
abiria aina ya Coaster linalofanya safari kati ya Ubungo, Tegeta katika
eneo la Tegeta Dar es Salaam.
Taarifa ya kituo cha ITV
imesema mafundi gereji wa Tegeta walifanya jitihada kutumia vifaa vyao
kukata mabati ya gari ili kuwatoa watu walionasa ndani ya gari iliyokuwa
na abiria.
Kamanda wa Polisi Kinondoni, Kamilius Wambura amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuahidi kutoa taarifa zaidi kuhusu baadaye baada ya uchunguzi kufanyika.
ConversionConversion EmoticonEmoticon