Afroman na kesi ya kupiga shabiki wa kike, hapa iko video ya tukio..

DSC_8978cAfroman ni mmoja ya mastaa waliowahi kusikika wakifanya poa kwenye muziki kutoka Marekani, lakini tukio alilolifanya safari hii limewashtua wengi, hawajalipenda kiukweli.
Jamaa alikuwa stejini akifanya show ikatokea shabiki wa kike akapanda stejini, Afroman aligeuka na kumpiga ngumi usoni halafu akaendelea na show yake, yule shabiki alianguka kwenye stage na kuumia.
Mtu wa karibu na Afro amesema jamaa hakujua kama shabiki huyo ni mwanamke, chini ya stage hakukuwa na ulinzi mzuri hivyo anaamini kitendo cha Afroman kilikuwa cha kujihami.
Polisi walimdaka jamaa na baadaye akaachiwa kwa dhamana ya dola 330 ambayo ni sawa na laki sita Tshs.
Tazama video ya tukio hilo hapa kwa kubonyeza play.
Previous
Next Post »