Askari wote wameshatawanyika eneo la Tukio na walichokuta ni Pikipiki, baiskeli, vyakula na nguo.

Hadi sasa taarifa kutoka mkoani Tanga zinaeleza kuwa askari wanne wa Jeshi la Polisi Tanzania wamejeruhiwa katika mapambano dhidi ya vikundi vya kihalifu (kigaidi) katika eneo machimbo ya Amboni mkoani humo. Taarifa zaidi zinasema askari hao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga kwa matibabu zaidi na kuna watu wawili ambao wamekamatwa kuanzia jana hadi sasa wakihusishwa na tukio hilo. Aidha, mmoja wa Askari waliopo katika eneo la tukio amesema mapema leo asubuhi Helkopta ya Polisi ilinusurika kudunguliwa na vikundi hivyo vinavyosadikiwa kuwa viko zaidi ya vinne. Pamoja na ulinzi kuimarishwa kila kona ya eneo hilo imeelezwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoani Tanga atatoa taarifa ya tukio hilo saa 15:00pm. UPDATES II: Pango walimojificha magaidi limevunjwa kwa kutumia mizinga, na hatimae jamaa wametoroka hakuna aliekamatwa, Sergeant Kajembe wa JWTZ aliepigwa risasi ya Tumbo ameshafariki Dunia, majeruhi waliopo hospital ni PC mmoja wa FFU, Sergeant wa JWTZ aliejeruhiwa sikio, Corporal alijeruhiwa mguu.

Previous
Next Post »