Diamond: Ningekuwa na Sauti Kama ya Ally Kiba, Ningefanya Makubwa Zaidi

Diamond Vs Ali Kiba ni ushindani usio rasmi unaochochewa zaidi na mashabiki wa muziki Tanzania kwa kuwa wawili hao licha ya kuwa wote ni wasanii wenye uwezo mkubwa sana kwenye uimbaji wanatajwa kuwa na tofauti au vita baridi.


Wapo wengi ambao wanauzungumzia hata kama sio kwenye vyombo vya habari na kuna wachache ambao maoni yao yamefika kwenye vyombo vya habari.

Vijimambo imezungumza na mmiliki wa G Records, Guru Ramadhani aka DJ G-Lover ambaye studio yake ndiyo ilimtoa Ally Kiba na kumfikisha kwenye mkondo mkubwa wa muziki ametoa maoni yake kuhusu utofauti anaouona kati ya wasanii hao.

Guru anaamini kuwa Ali Kiba ana hazina kubwa ya sauti na anakumbuka kuwa Diamond aliwahi kuisifia.

“Kwa kweli tofauti ukija kwenye masuala uimbaji, wengi wanaongelea hata katika mitandao tofauti tofauti kwamba Ali ana sauti nzuri na anaimba vizuri. Hata Diamond kuna wakati alikuwa anakiri kwamba angekuwa ana sauti kama ya Alikiba basi angefanya mambo makubwa zaidi.” Amesema G-Lover.

Kwa mujibu wa G-Lover, wakati Ally Kiba yuko juu kupitia studio yake alikuwa na team ya watu wasiopungua thelathini, kitu ambacho Diamond anakifanya sasa hivi.
Previous
Next Post »