Dully Sykes: Sishangai ugomvi wa Alikiba na Diamond, nashangaa wa TID na Q Chillah

Dully Sykes amedai kushangazwa kusikia watu wazima kama TID na Q Chillah wakilumbana kwa jambo la miaka mingi iliyopita na kwamba mambo kama hayo wanapaswa kuwaachia wadogo zao mathalan Alikiba na Diamond.
Dully ameiambia Bongo5 kuwa TID na Q wamemfedhehesha.

“Hawa ni watu wazima,” amesema Dully. “Mimi kama kuwazungumzia ninawazungumzia Diamond na Alikiba. Hawa ni vijana, kwanini Q Chillah na TID wasimalize masuala yao? Wanashindwa kuweka pembeni tofauti zao! Kwanini wanagombana wakati ni watu wazima tayari?

“Sishangai ugomvi wa Alikiba na Diamond nashangaa ugomvi wa TID na Q Chillah kwasababu Diamond na Alikiba ni watoto! Mimi nitashangaa TID kugombana na Q Chillah kwasababu wao ni watu wazima. Wanatakiwa wapatane ili watoto kama Diamond na Alikiba wapatane. Mimi siwezi kuzungumza nao chochote waache wagombane.”
Previous
Next Post »