Iyobo Ashikwa na Kigugumizi Kuhusu Mume wa Aunt Ezekiel

Mcheza Dansi wa mwanamziki  Diamond, Mose Iyobo ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ameshikwa na kigugumizi kuhusu tuhuma za kumpachika mimba Aunt ambaye ni mke wa mtu.

Mose alionesha kigugumizi hicho baada ya kutaitiwa na paparazi wa GPL akiulizwa anajisikiaje kumpachika mimba mke wa mtu na vipi kama mume wa Aunt anayedaiwa kufungwa huko Dubai ataachiwa huru na kurudi.“Aaahhaa.. Mhh..Hayoo ni ya Aunt mwenyewe mimi hayanihusu,” alisema Mose kisha kimya kirefu kikafuatia kabla ya kuikata simu yake.
Previous
Next Post »