Picha: Crazy GK aingia studio na Vanessa Mdee kuandaa ngoma mpya

Msanii wa East Coast Team, King Crazy GK ameingia studio kurekodi ngoma mpya na Vanessa Mdee.

Kazi hiyo mpya inayoandaliwa na mtayarishaji mkongwe, John Mahundi akishirikana Marco Chali, inasimamiwa na AY.

“Yeah mzigo upo jikoni na soon utausikia maskioni,” GK ameiambia Bongo5. “Sidhani kama itaathiri kutoka kwa kazi za East Coast ila inawezekana kwasababu huwezi kuachia kazi mbili kwa pamoja, lazima moja ianze kwanza na nyingine ifuate,” ameongeza.

“Beat kila kitu kimeandaliwa na John Mahundi na Vanessa ndo anaingiza vocals kwa Marco Chali. Kiukweli hii kazi imesimamiwa kila kitu na AY na baada ya hapo hii project itatoka.”

GK amesema anamshirikisha Vanessa kwakuwa ni muimbaji wa kike anayemkubali zaidi.

“Unajua Vanessa ni hatari sana kwenye muziki, ana uwezo mzuri sana ndio maana ukamuona kwenye hii project yetu.”
Previous
Next Post »