Lulu Michael Azua Jambo Kwa T-Shirt Aliyovaa Siku ya Valentine

Mara kadhaa tume kuwa tukiwaona  baadhi ya ndungu zetu ambao Lugha ya malkia inawapiga chenga wamekuwa wakivaa nguo zenye maandishi ambayo huwa hayafai lakini hawa mara nyingi huwa hawajui maana ya kile ambacho kimeandikwa.



Sote tunatambua kuwa watu wenye uelewa kama wa mrembo huyu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hawezi kuvaa ngue yenye maandishi akiwa ajui maana yake au hakubaliani na kile kilichoandikwa. Sasa je mtoto lulu ni kweli  anamaanisha hiki kilichoandikwa hadi kupiga nacho picha na kutupia mtandaoni. Au labda ni dili amepata la kutangaza kinywaji.

Kama sio,ndio tuseme kweli mrembo huyu anapenda kilaji kiasi kwamba haitaji kupendwa na mtu yoyote?

Hebu tuambie wewe umemuelewaje hapa bidada huyu.
Previous
Next Post »