PICHA: Timbwili Mitandaoni, Diamond Akiwa na Zari Huku Wema Akiwa na Ommy

Kweli mafahari wikigombana nyasi ndio uumia! Picha za mwanamziki Diamond akiwa na mpenzi wake Zari  wakiwa ndani ya gari alizoziweka mtandao usiku wa kuamkia jana siku ya wapendanao na kuandika kwa maneno ya lugha ya kingreza kuwa wanaelekea siku ya Valentine “Road to Valentine...”
Zilizua timbwili la maneno miongoni mwa mashabiki wa Diamond ambao walikuwa wakisifia
“Project hii” na wale wa Wema  aka TeamWema walikuwa wakiponda na kumshabulia sana mwanadada Zari ikiwemo kumuiga mtindo wa nywele Wema. Hii ilipelekea watu kutupiana maneno makali na mazito yanayoweza kukufanya msomaji upofuke macho.

Baada ya mvutano mrefu kuhusu picha hizo za Diamondi na Zari, Ikatupiwa picha hiyo ya Wema akiwa na Ommy, hapo tena moto ukawaka wale wa mashabiki wa Diamond wakaanza kuponda huku TeamWema wakisifia. Mwisho wa siku watu wakaamua kuzileta pamoja ili watu waseme bila ushabiki kuwa ipi ni project ya ukweli na ipi feki….


Nami nikaona nizilete hapa kwenu,ila sio kushindanisha bali upate kuziona na kukupa ubuyu wa kile kinachoendelea kuhusina na picha za mafahari hawa wawili wenye mashabiki wengi zaidi hapa Bongo.

Jamani mashabiki acheni kutukanana huko mitandaoni, mbona wenyewe hatukanani?

Mzee wa Ubuyu
Previous
Next Post »