POLE SANA CHRIS BROWN MWENZAKO NILICHEKWA - OMMY DIMPOZ

Msanii Omary Nyembo alimaarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kusema kuwa watu wa uhamiaji duniani kote huwa hawatambui umaarufu wa mtu pindi wanapogundua kuna kitu hakijaenda sawa,Ommy Dimpoz amefunguka hayo leo kapitia ukurasa wake wa
Intrgram baada ya mwimbaji kutoka Marekani Chris Brown kuzuiliwa kuingia Canada na kusababisha kusitishwa kwa show zake mbili ambazo alitakiwa kuzifanya Canada ndani ya wiki hii.
Ommy Dimpoz ameonyesha njisi gani watanzania na mashabiki wake walilipokelea suala lake tofauti na kuonyesha kuwa watu wengi walimcheka na kumchamba wakiamini kuwa yeye ni mtu maarufu hivyo asingeweza kupatwa na suala hilo.
"Pole braza Kristofa, haya ni Mambo ya kawaida ila Mwenzio nilivyozuiwa kuingia Nchini kwenu Basi nilivyorudi kwetu nimechekwaaa,Nimechambwaa khaa,hawajuagi mambo ya Uhamiaji hawajali we nani."
Wiki ya wapendanao msanii Ommy Dimpoz alirudishwa Tanzania baada ya kuzuiwa kuingia Marekani kwa kukosa vibali vinavyomruhusu kuingia nchi hiyo kufanya show
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Previous
Next Post »