Jumatatu ya February 9 nimekuwekea U Heard ya leo ambayo inahusu tetesi za wasanii wakike Vanessa na Shaa kuonekana kutokuwa na maelewano kati yao katika show iliyofanyika hivi karibuni huku ikisemekana kuwa wanashare dancers hivyo kuwa na mvutano kila mmoja kutaka awe wa kwanza kuwatumia.
Soudy Brown alikutana na wasanii hao hivi karibuni wakiwa katika show kwa upande wa Shaa amesema kuwa hawana ugomvi wowote kwani wasanii wakike wako wachache kwa hiyo hawaoni haja ya kugombana.
Vanessa nae amefunguka kuwa wanapeana support ili waweze kufika mbali, kuhusu dancers hao Vee
amesema wako vizuri ndio maana wanawatumia wote kwa pamoja, hawana haja
ya kugombana kwani watu wanataka kuwagombanisha ili washindwe kufanya
muziki na kupotea kwenye ramani.
Bonyeza play kuweza kusikilia U Heard ya leo February 9.
2 comments
Click here for comments(o)
Reply:-)
ReplyConversionConversion EmoticonEmoticon