WASTARA AWACHARUKIA WANAOMTUSI MUMEWE


MSANII mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Wastara Juma ameapa kumshtaki mtu atakayekamata kutokana na baadhi ya mashabiki kuwa na tabia ya kumtukana matusi ya nguoni mtandaoni huku wakimhusisha na marehemu mumewe, Sajuki.
Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Wastara Juma.
Akizungumza na gazeti hili, Wastara alisema anajisikia vibaya baadhi ya mashabiki wanavyomtukana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo siyo zuri kwani wanaingilia maisha yake binafsi na kibaya zaidi wanamhusisha Sajuki.
“Ukweli sipendi kabisa na nitamshtaki mtu maana wananitengenezea chuki kwani wakati mwingine wananitukana, wanamtukana sana Bondi huku wakidai kwamba nilikuwa naomba Sajuki afe ndiyo nifanye mabaya sasa sijui nimefanya kitu gani kibaya, kuwa na Bondi nimekuwa naye baada ya mume wangu kufariki maana mimi ni binadamu na kama angekuwepo nisingekuwa na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema Wastara.
Previous
Next Post »