ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KURIPOTI KWA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI KESHO KUTWA KUTOA MAELEZO


Wakati Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akijisalimisha kwa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka alipoti ofisini kwake kesho kutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini
Makonda amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.
Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. 
“Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini.”
Gwajima alipoteza fahamu jana alipokuwa akihojiwa na Polisi kwa tuhuma za kumkashfu Kardinali Pengo.
Previous
Next Post »