EL CLASICO: MATHIEU, SUAREZ WAPELEKA KILIO REAL MADRID

Luis Suarez akishangilia bao aliloifungia Barcelona na kuipa ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Madrid usiku huu.
Lionel Messi akijaribu kuwatoka wachezaji wa Real Madrid wakati wa mechi hiyo.
Cristiano Ronaldo akiifungia Real Madrid bao pekee katika dakika ya 31 ya mchezo.
Jeremy Mathieu akipiga mpira wa kichwa uliozaa bao la kwanza kwa Barcelona.
MABAO mawili yaliyofungwa na Jeremy Mathieu katika dakika ya 19 na Luis Suarez dakika ya 56 yameipa ushindi timu ya Barcelona dhidi ya mahasimu wao Real Madrid kwenye uwanja wao wa nyumbani Nou Camp usiku huu.
Katika mtanange huo wa La Liga, Barcelona wametoka kifua mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid.
Bao la Real Madrid limewekwa kimiani na Cristiano Ronaldo dakika ya 31 ya mchezo.
Kwa matokeo hayo, Barcelona wamefikisha pointi 68 mbele ya Real Madrid wenye pointi 64.
Previous
Next Post »