MENINA,BABA LEVO LIVE


Live! Mastaa wawili wa Bongo Fleva, Menina Atick na Baba Levo wamenaswa kimahaba hivyo kuibua viulizo kuwa huenda kuna ‘projekti’ inaendelea kati yao.
Katika tukio hilo ambalo Baba Levo alishuhudiwa ‘akijibebisha’ kwa Menina lilijiri kwenye Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar ambapo wawili hao walijumuika na wasanii wenzao katika hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Ishi Kistaa iliyokuwa ikichukua nafasi ukumbini hapo.
 Meninah la diva akiwa katika pozi.
Wakati burudani na mambo mengine yote yakiendelea mahali hapo, Baba Levo na Menina walijitenga wakaenda kubana chobingo na kuanza kufanya yao.
Baada ya kuwaona, mwanahabari wa Ijumaa Wikienda aliwafuata wawili hao ili kujua kulikoni uwepo na ukaribu wao mahali hapo tena wakiwa chemba ambapo Baba Levo huku akicheka alijibu kuwa kwani yeye hafanani kuwa na mtoto mkali mwenye mvuto kama Menina!
Previous
Next Post »