Picha: Wema Sepetu Kwenye Uzinduzi Rasmi wa Mitsubishi ASX, Mashabiki Wake Wampongeza

Wema Sepetu Hizi ni baadhi ya picha  za mrembo na staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu hapo jana usiku  katika uzinduzi rasmi  wa gari la kampuni ya Mitsubishi aina ya ASX  akiwa kama balozi.

Hivi karibuni Wema Sepetu na mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo, walipata shavu la kutengeneza tangazo la  gari hilo jipya  ambapo kwenye tangazo la gari hilo, mastaa hao wenye ushawishi mkubwa wanaonekana wakisifia vitu mbalimbali vilivyomo kwenye gari hilo.

Katika Hatua Nyingine Mashabiki wake wamefurahishwa na Jinsi Wema Anavyojituma kwa sasa kwenye Kazi mbalimbali Kwa kutumia Jina na Umaarufu wake kujiongezea kipato tofauti na alivyokuwa na Diamond..

Hongera sana Wema na team yako kutoka Endless Fame
Previous
Next Post »