Sugu "Kikwete Studio Uliyoitangazia Dunia Kawapa Wasanii iko wapi na Umemkabithi Nani?'

Joseph Mbilinyi aka Sugu Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, amesema hajaweza kufanya kitu chochote kuwasaidia wasanii kwa kuwa wakati anagombea Ubunge hakuna aliyekuwa nyuma yake. Sugu amelazimika kusema hayo baada ya shabiki kutaka kujua ni kitu gani alichowafanyia wasanii tangu awe Mbunge.

''Hao wanaozingua wakamuulize Kikwete studio aliyoitangazia dunia kawapa wasanii iko wapi na kamkabidhi nani, amehoji Sugu kwenye Instagram. Rais kashindwa kuwasaidia wanataka kumlaumu mbunge wa Mbeya mjini, wakati hata hao wasanii wenyewe kimsingi hawakutusapoti kwa namna yoyote wakati tunagombea huo ubunge, wote walikuwa wanajipendekeza kwenye kampeni za CCM''.
Previous
Next Post »