Mwanasiasa
kijana, Zitto Kabwe, amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama kipya cha
siasa cha upinzani ACT Wazalendo, katika uchaguzi uliokamilika usiku wa
kuamkia leo Jumapili Machi 29, 2015.Kwa mara ya kwanza chama hicho
ambacho katika katiba yake, kinaonyesha patakuwa na viongozi wakuu,
wakiongozwa na kiongozi wa chama, mwenyekiti wa chama, makamu wenyeviti
wawili kutoka bara na visiwani, katibu mkuu, na manaibu katibu wakuu
wawili kutoka pande zote za muungano kitakuwa chini ya uenyekiti wa
mwana mama Mwanasheria msomi.
Matokeo hayo yanaonyesha, mwanamama huyo,
Anna Mghwirim, ndiye aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa taifa wa chama
hicho, makamu mwenyekiti bara, Shaban Mambo, na makamu mwenyekiti
Zanzibar, Ramadhan Suleiman Ramadhan.
Katibu Mkuu na manaibu wake, wanasubiri
mapendekezo ya kamati Kuu ya chama ambayo ilitarajiwa kukamilisha kazi
yake mapema alfajiri ya Jumapili. Pichani kiongozi huyo wa chama, Zitto
Kabwe, akilakiwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, wakati wa
uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye ukumbi wa Kadinali Rugambwa, Oysterbay
jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 28, 2015. Zitto alichaguliwa kuwa
kiongozi wa chama hicho nafasi ambayo kwa katiba ya chama hicho ndiyo ya
juu zaidi. Chama hicho kitazinduliwa rasmi Jumapili Machi 29, 2015
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
Zitto akionyesha alama ya chama ambayo ni "Uwazi"
Zitto akihutubia wajumbe
Zitto akihutubia wajumbe wakati wa uchaguzi huo
Zitto akipongezwa
Wajumbe wakiserebuka, wakati wa uchaguzi huo
Wajumbe wakifurahi kwa kushikana mikono kuonyesha umoja
Wajumbe wakipiga kura
Askofu Gerald Mpango akiongoza sala
Mzee Kastiko, akiw
ConversionConversion EmoticonEmoticon