Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa amewaahidi wafuasi
wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema pamoja na wale wa umoja wa
katiba ya wananchi (UKAWA) ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika oktoba 25 mwaka 2015.
Lowassa alisema hayo jana mara baada ya kukabidhiwa fomu ya
kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Demkorasia na Maendeleo ambayo
itampa ridhaa ya kugombea urais kupitia umoja wa Katiba ya wananchi
ukawa unaundwa na vyama vinne vya siasa nchini Tanzania ambavyo ni
Chadema, NCCR-Mageuzi, Cuf na NLD.
Aidha, Lowassa aliyekabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe katika ofisi za
Chadema makao makuu yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam
jana,alichangiwa kiasi kadhaa cha pesa kitakachomsaidia katika yake ya
matumaini iliyofufukia Ukawa. Katika hafla hiyo Lowassa aliongozana na
Mkewe pamoja na wana familia na ndugu wengine mbalimbali.
Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba ili
mgombea ameweze kuwania urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni
lazima awe mwanachama wa chama chochote cha Siasa nchini Tanzania, hivyo
Lowassa ni mwanachama halali wa Chadema pia amechaguliwa na vikao
mbalimbali vya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi hadi usiku wa manane.
Uamuzi wa Lowassa kugombea Urais ulipokelewa kwa shangwe na
umati wa wananchi uliohudhuria hafla hiyo makao makuu ya Chadema
kinondoni jijini Dar es salaam.
Mwanasiasa huyo Mkongwe atapambana na Mgombea kutoka chama
cha Mapinduzi Dk.John Magufuli katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu
utakaokuwa wa aina yake mwaka huu wa 2015.
ConversionConversion EmoticonEmoticon