Tukio la MTV Video Music Awards limekuwa likichukua headlines kwenye vitu tofauti, headlines zake bado ziko nyingi zinazosambaa kwenye mitandao.
Licha ya watu wengi kuchukua tuzo na kupendeza kwenye usiku wa MTV VMAs za
mwaka huu, kumekuwa na tetesi nyingi zinazosambaa kwenye mitandao kuwa
kutokana na watazamaji kuwa wachache mwaka huu show hiyo kubwa ya tuzo
za muziki Marekani ziko hatarini na pengine tuzo za mwaka huu ndio za mwisho.
So hii inamanisha kuwa tuzo za MTV VMAs za Marekani ndio zimefika mwisho? Mike Jafar Makamu Rais wa mawasiliano ya kampuni ya Viacom
amekanusha tetesi hizi na kusema chochote kile kinachosambaa kuhusu
tuzo hizo ni taarifa ambazo hazina ukweli wala ushahidi ndani yake.
Tuzo za MTV Music Awards maarufu kama MTV VMA’s zimekuwa zikiruka kila mwaka toka mwaka 1984, na mwaka huu show hiyo imetimiza msimu wake wa 32… Kuhusiana na watazamaji kupungua Mike Jafar alisema kuwa watazamaji hawajapungua na kwa mwaka 2014 tu tuzo hizo zilipata ongezeko la watazamaji kwa 18%.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi
ConversionConversion EmoticonEmoticon