Serikali imetenga Trilioni 1 za kukopesha

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga Tsh. Trilioni moja kwa ajili ya mikopo kwa mabenki na taasisi za fedha kwa riba ya asilimia tatu ili mabenki na taasisi hizo zitoe mikopo kwa riba isiyozidi asilimia 10. “Serikali imeendelea kulegeza masharti ya uanzishwaji wa ofisi za wakala wa mabenki, kushusha riba inayolipwa kwa akaunti za fedha za mitandao pamoja na kutenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya mikopo kwa mabenki na taasisi za fedha kwa riba ya asilimia tatu ili mabenki na taasisi hizo zitoe mikopo kwa riba isiyozidi asilimia 10″ Ametoa kauli hiyo jana wakati akiahirisha Mkutano wa Tano wa Bunge Dodoma, Bunge limeahirishwa hadi Februari mosi, mwakani, Majaliwa amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2022/2023. Akizungumzia kuhusu, riba kubwa za mikopo kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha, Waziri Mkuu amesema Serikali imekuwa ikichukua hatua madhubuti kupitia Benki Kuu ya Tanzania ikiwemo kupunguza kiwango cha akiba kinachowekwa na mabenki katika Benki Kuu.
Previous
Next Post »