Kwa muda wa kama wiki mbili kumekuwa na story juu ya kuvunjika kwa uhusiano ya mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo na mpenzi wake ambaye ni mwanamitindo, Irina Shayk.
Wiki iliyopita msemaji rasmi wa Irina Shayk alithibitisha kwamba mrembo huyo mwenye asili ya Urusi ameachana na Ronaldo
ambaye alikuwa na uhusiano naye kwa muda wa miaka 5, hata hivyo tetesi
juu ya chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano huyo zikaendelea huku mama
mzazi wa Cristiano Ronaldo akitajwa kuhusika.
Mama mzazi wa Ronaldo, Dolares ametajwa kumkataa Irina kwa sababu haoni kama mwanamke huyo atafaa kuwa mzazi mwema kwa mtoto wa Ronaldo aitwaye Cristiano JR.
Hata hivyo baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye Cristiano Ronaldo ameibuka na kuthibitisha kwamba ameachana na Irina huku akiomba jamii imuache aendelee na maisha yake binafsi.
Katika taarifa aliyotoa leo kwa vyombo vya habari, Ronaldo alisema ; “Huu ni mwisho wa uhusiano wangu na Irina Shayk baada ya kudumu kwa miaka mitano. Tunaamini uamuzi huu ni sahihi kwa wakati huu“
ConversionConversion EmoticonEmoticon