Msanii
maarufu nchini mwenye mafanikio makubwa katika sanaa ya mziki wa kizazi
kipya, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake juu ya ubovu wa barabara
iendayo Madale ambayo ipo kwenye jimbo la Kawe chini ya Halima Mdee.
Msanii
huyo ameelekeza lawama zake kwa mbunge huyo wa kupitia tiketi ya
CHADEMA kwa kuwa Halima Mdee aliahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa katika
kipindi chake cha ubunge atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa
kiwango cha lami, lakini hadi hii leo barabara imejaa tope tu!
Diamond
alieleza masikitiko yake huyo kupitia katika kituo cha Clouds TV pale
alipoulizwa swali kuhusu makazi yake mapya yaliyopo katika jimbo la Kawe
na ndipo hapo akafunguka kuhusu suala hilo la kero ya barabara ambalo
lina muda mrefu alijashughulikiwa na mbunge Halima Mdee.
ConversionConversion EmoticonEmoticon