Just thinking loud!
Sasa
anafanya safari juu ya safari, mikutano juu ya mikutano, facebook,
twitter, kukutana na waandishi wa habari usiku wa manane, nk. Kiongozi
huyu mkuu kwa sasa halali, hatulii, wala hasikii la mkuu.
Najaribu
kuvuta taswira nyuma kidogo, wakati akiwa chama kilichomlea, chama
kilichomfikisha hapo alipo sikuziona jitihada hizi. Wakati huo, wenzake
wakifanya mkutano Arumeru, yeye alikwenda kula bata Germany. Wakati
wakiendelea na M4C, yeye alikuwa Uswizi akisaka kwa udi na uvumba majina
ya waliohifadhi fedha huko. Sababu hazikuisha ilimradi tu jina na sura
yake isionekane katika timu ya ukombozi.
Ninachojiuliza,
kazipata wapinguvu hizi za ziada, ambazo siku chache zilizopita hakuwa
nazo. Ukisoma alama za nyakati, low profile ya wakati huo na high
profile ya wakati huu utajiuliza maswali na utapata hisia, hisia za
usaliti. Deal lilipangwa kitambo kwa siri likabumburuka, akaenda
mahakamani. Kwa sasa ni utekelezaji wa deal hilo kwa hisani ya watu wa
Marekani, naamini nalo litabumburuka.
Kama
Taifa hili lingekuwa la uwazi na ukweli, na kama ofisi ya mkaguzi wa
hesabu za serikali angeweza kutupia jicho, tungetaka kufahamu juu ya
mapato na matumizi ya chama hiki kwa miezi mitatu tu iliyopita. Term of
reference zingekuwa nini vyanzo vya mapato ya Matangazo ya moja kwa
moja, safari ya kusini, na kama mapato haya yanaripiwa kodi *income
tax*
Mtu
aweza kujiuliza, pamoja na madeni kwenye asasi za fedha, je ni kweli
Milioni 5 zilizotangazwa kama salio la account ndizo zinagharamia
mikutano na safari hizi kibao.
Democrasia inapokwa kwa watu kukubali kutumika kwa masilahi yao binafsi!
By Rpg-JF
ConversionConversion EmoticonEmoticon