Nay wa Mitego aeleza kwanini alinunua sanamu ya shetani kwa shilingi milioni 5

Nay wa Mitego ni mtu wa maamuzi na mapenzi tofauti na wengine. Ndio maana ukiingia ndani kwake utakutana na sanamu isiyo ya kawaida – ni sanamu ya shetani!

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa sanamu hiyo ni moja ya vitu anavyovipenda zaidi ndani mwake.

“Mimi naipenda na niliinunua hela nyingi tu, ni dola elfu tatu,” amesema Nay.

“Nilitokea tu kuipenda, ni moja kati ya vitu muhimu ninavyovipenda ndani ya nyumba yangu. Kuna sehemu niliinunua sio Tanzania. “Mimi nilitokea kukipenda yaani naipenda sana tena sana na hata ukiingia ndani kwangu utaanza kuiona hiyo,” amesisitiza rapper huyo.
Previous
Next Post »